[SWA] Sekta ya Mchezo wa Video 2021 | Mazungumzo na Jay Shapiro
English Version Here
Hata nje ya sekta ya mchezo wa video, Afrika haizungumziwi sana kama inavyotakiwa. Bara linalochipukia kwa namna yake katika nyanja mbalimbali limerudishwa nyuma kwa haraka sana na nchi na mataifa makubwa, kwa sababu ya kutokuwa na ufahamu wa kiuchumi kwa maswali kama vile “Je, watumiaji wa Kiafrika hata wana simu za mkononi kweli?” au “hivi intaneti ya broadband si hata haipo huko?” Ni kauli kama hizi mbovu ambazo zinazuia sehemu yenye utajiri kama Afrika isizungumzwe kwa picha nzuri kama inavyostahili.
Hakuna mtu anayefahamu hili vizuri zaidi ya Jay Shapiro, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Usiku Games na mjasiriamali mahili. Shapiro, Mkanada mwenzangu, amekuwa na kazi nzuri hadi sasa. Baada ya kumaliza Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Biashara (MBA) Chuo Kikuu Cha Taifa Singapore katika Masoko, alianzisha kampuni ya BLUE mnamo mwaka 1999, kampuni ya matangazo ya kidigitali ambayo baada ya miaka 8, na kufungua ofisi zake London, NYC, Shangai, Palo Alto na Tokyo (tukitaja baadhi tu ya mijiji), ilifanikiwa kuwa kampuni ya matangazo ya kidigitali ya nne kwa ukubwa duniani kwa wakati huo. Sio jambo la kushangaza kwamba WPP walikuwa na shauku ya kuinunua kampuni hiyo mnamo mwaka 2007. Baada ya Shapiro kukimbia hali ya hewa ya unyevunyevu iliyopo Kusini Mashariki mwa Asia na kuhamia Mji wa New York, ambako alianzisha kampuni ya Appmakr kwa miaka 8, wachapishaji wenye mafanikio wa app za simu, ambayo aliiuza mwaka 2019.
Safari yake ya kusisimua ya hivi karibuni ilimpeleka Nairobi, Kenya alipoanzisha Nairobi Game Development Center na Usiku Games. Tutajifunza zaidi juu ya kampuni hizi katika sehemu ya pili. Lakini kwanza, ninataka kukushirikisha mambo makubwa niliyopata fursa ya kuyasikia kutoka katika video ya hivi karibuni ya Jay. Mambo haya yanaweza kuwekwa katika makundi manne.
Afrika kama bara
Kutoka Michezo ya Kubashiri mpaka Michezo ya Video
Kulea Kipaji cha Utengenezaji wa michezo ya video
Kwenye Upeo wa Macho
Afrika kama Bara
Viashiria vya Kiuchumi
Tofauti na mabara mengine kama vile Ulaya au Amerika Kaskazini, kuna hamu inakuwepo ya kuitazama Afrika kwa mtazamo mmoja. Kuitazama kama eneo moja tu la kijiografia ambalo halina mipaka ya kitamaduni au kiuchumi baina ya nchi zake 54 na lugha 2000. Hata ukitazama kwa haraka tu viashiria vya maendeleo ya kiuchumi na kibinadamu kama vile GDP au kiwango cha elimu vinaweza kubatilisha dhana hii na kuonyesha ni wapi tunapoona ukuaji mkubwa zaidi.
Maana yake ni kwamba wakati CNBC au The Economist wanataja Afrika wanakuwa kwa kiasi kikubwa hawamaanishi maeneo kama Somalia au Chad lakini wanakuwa wanaangalia maeneo kama Nigeria, Kenya au Rwanda ambayo yanaukuaji mkubwa wa YoY GDP, yakiongoza ukuaji wa teknolojia na elimu. Fahamu ya kwamba nikitaja Afrika kwa ujumla katika andiko hili ni kwa ajili ya ufupisho tu ili nisiorodheshe masoko yote yanayokua yaliyopo katika bara hili.
Kiashiria kidogo ambacho hakionekani sana kinachoonyesha namna bara la Afrika limefanikiwa kiuchumi ni katika piramidi ya idadi ya watu wake. Afrika ni changa, change sana. Tazama piramidi hapo chini zikilinganisha Kenya dhidi ya China.
Piramidi ya Idadi ya Watu Mwaka 2019 ya China & Kenya
Piramidi ya idadi ya watu wa Kenya inaashiria kwamba kwa ujumla wake, vijana wengi wa Kenya hivi karibuni wataingia katika miaka yao ya ubora kiuchumi (Miaka 22 - 60). Watakuwa na shahada za chuo, kipato cha ziada, wataanzisha familia, watawekeza na kulipa kodi. China inapitia kipindi hiki cha juu hivi sasa kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wake wakiwa katika miaka ya kuchangia katika uchumi. Hata hivyo ndanin ya miaka 20-30 China itapitia kipindi cha kupungukiwa kwa wingi. Kizazi chake cha nguvu kazi, walio kazini hivi sasa, watakuwa na umri mkubwa na kumaliza rasilimali zao kwa mfumo wa pensheni, fedha za kujali wazee na kiujumla watatumia bidhaa na huduma kwa kiwango kidogo zaidi ukilinganisha na kipindi cha nyuma.
Kama unataka kujua zaidi juu ya piramidi ya idadi ya watu katika nchi yako - tazama link hii!
Bilioni Inayofuata
Tofauti na India na China, Afrika ndiyo jibu pekee la swali gumu la: “Watumiaji bilioni wanaofuata watatoka wapi”. Ndani ya bilioni hao, mamia ya mamilioni ya vijana wa Afrika, haswa katika masoko muhimu kama Kenya, Nigeria, Ethiopia au Senegal hivi karibuni watakuwa wachangiaji wakubwa kiuchumi wakiwa na kipato cha ziada, mifumo bora zaidi ya malipo ya simu na simu zinazoweza kucheza michezo ya video simu ya kisasa. Haya yote yanawezeshwa na mtandao wa simu wa 4G (na 5G inayozidi kukua) ambao una ubora zaidi na gharama nafuu. Upatikanaji wa Cloud computing pia sio ni mzuri, huku Microsoft Azure na seva za AWS zikipatikana barani kote.
Jifunze zaidi juu ya Makao Makuu ya Amazon nchini Afrika Kusini
Mchanganyiko huu mzuri wa idadi ya watu, maendeleo ya miundombinu na uwekezaji wa mataifa ya nje unatengeneza mustakabali mzuri kwa masoko ya Afrika huko mbeleni. Je, vipi kuhusu michezo ya video?
Kutoka Michezo ya Kubashiri mpaka Michezo ya Video
Hali Ilivyo
Jay Shapiro alipokuja Nairobi aligundua bango la barabarani moja baada ya lingine. Yote yakitangaza huduma moja ya mchezo wa kubahatisha – SportPesa.
SportPesa ni kampuni ya michezo ya kubashiri na inafanana na nyingine nyingi zilizopo Kenya:
Makampuni haya kimsingi yanamilikiwa na Wachina au Wamalta na hii inamaanisha kwamba pesa inaondoka nje ya Afrika haibaki ndani.
Watumiaji Hai Kila siku 1M+ wakiweka kwa wastani beti 3+ kwa siku
Wakazi wa maeneo duni ambao hupoteza kiasi kikubwa, mara nyingi au hushinda kiasi kidogo mara chache
Hesabu za haraka zinaonyesha kwamba 1 USD x Beti 3 kwa siku x Watumiaji 1M = $3m USD ya betting kila siku kwa SportPesa pekee. Haishangazi kwamba kwa ujumla michezo ya bahatinasibu ndani ya Kenya ilikuwa na thamani ya $37Bn mnamo mwaka 2013.
Namba kubwa kama hizi zinatuonyesha ukweli kwamba – watumiaji katika masoko ya Afrika yaliyoendelea wameshazoea michezo katika simu zao za mkononi. Na ni wazi michezo hii, inasisimua bila kujalisha upo Manhattan au katika makazi duni nchini Kenya. Mzunguko wa dopamine kutokana na kucheza michezo ni msingi wa binadamu yoyote, na hivyo makampuni ya Kichina na Kimalta yamegundua njia ya kuweka hilo jambo katika biashara kwa mfumo wa apps kama vile SportPesa.
Fursa
Hivyo michezo hii ina nafasi kubwa sana katika maeneo kama ya Kenya kwa mfumo wa kubashiri michezo ya video. Je, sekta ya michezo ya Kiafrika ikizaliwa upya itakuwaje? Inaondokanaje na zana ya “kuwa mwisho wa ubongo” inayotokana na michezo hii ya kibepari ya kubashiri na kuwa sekta endelevu ambapo michezo inatengenezwa kwa ajili ya Waafrika na Waafrika? Ni kwa namna gani watumiaji vijana, wenye simu za mkononi, wanaweza kufurahia kutokana na kuwa na ujuzi, na sio bahati, na kukuza kitu kilicho chanya? Hapa ndipo Usiku Games inapoingia.
Usiku Games
Tovuti yao inaweka wazi mambo 4 yanayotoa taarifa juu ya falsafa yao ya kubuni michezo ya video:
#1 Muhimu na inayoakisi maisha halisi na tamaduni za Kiafrika
“Ilikuwa ni muhimu sana kwetu kuwa na maudhui yaliyotengezwa ndani”- Jay Shapiro
Sawa na mashaka aliyokuwa nayo Shapiro juu ya Africa kutazamwa kama bara moja tu – kuwa na mchezo ambao ndani yake una dunia zinazowakilisha uhalisia uliopo kutasaidia kuongeza utumiaji iwapo mchezaji anaweza kuona mazingira anayoyatambua na kugusana nayo.
#2 Isiyo na Vurugu – Hakuna bunduki katika michezo yetu yote
“Kuna bunduki za kutosha duniani, haswa Afrika.” ~Jay Shapiro
Soko la michezo ya risasi limejaa, na limekuwa hivyo kwa karibu miongo 2 sasa. Licha ya mafanikio ya michezo ya risasi, haswa kwenye simu za mkononi, kama Fortnite, Call of Duty Mobile, na mchezo uliotangazwa hivi karibuni Apex Legends Mobile, hakika ni soko gumu kuingia na kushindana, ukiachilia mbali mambo ya maadili.
#3 Ujumuishi wa Jinsia – Duniani wanawake wanacheza michezo ya simu zaidi ya wanaume
Licha ya mchezo #1 Afrika kuwa michezo ya video ya kubashiri, 90% ya wachezaji wake ni wanaume.
Ukiunganisha hilo na ukweli kwamba duniani, 65% ya wachezaji wa michezo ya video ya simu ni wanawake ni wazi kwamba kuna fursa iliyo wazi ya kutengeneza michezo ya video inayowavutia wanawake.
#4 Ye Elimu – Aidha kwa kupitia ufikiriaji, au maada fulani maalumu
Elimu na michezo vinapokutana ni jambo la kuvutia na uamuzi wa kuwa na muundo huu unaweza kupelekea kutoa fursa kwa Usiku Games kuchezwa madarasani siku moja!
Ujanibishaji wa Mchezo
Kwa ambao hawafahamu, ujanibishaji wa mchezo ni mchakato wa kubadilisha mchezo ili uweze kutolewa katika masoko ambayo yanaongea lugha tofauti. Kwa mfano, Nintendo wanaweza wakatengeneza mchezo wa Legend of Zelda mjini Kyoto, Japan lakini utatumwa kwa timu iliyopo Redmond, Washington kwa ajili ya kutafsiri maandishi ndani ya mchezo kuwa ya Kiingereza, kubadilisha vitu vidogo vya kitamaduni au wakati mwingine kuondoa maeneo ya mchezo yanayoweza kuonekana hayafai kwa masoko ya ulaya.
Ni hadithi kama hizi ambazo zinaonyesha kwamba ujanibishaji ni zaidi ya kile tunachokifikiria tu. Sio tu maandishi, lakini huanzia katika misingi, na namna mchezo unavyoweza kuwasiliana na mchezaji.
Shapiro anaamini ya kwamba suala hili linaenda mbele zaidi ya muundo wa mchezo tu na kutumika katika uuzaji pia akisema kwamba 92% ya watu wa Afrika wanalipia kwanza na kisha kutumia simu, na sio kulipia baadae kama ilivyo nchi za magharibi. Linapokuja suala la namna mpya ya kulipia michezo ya video (mfano Xbox Games Pass), makampuni yanatakiwa kufahamu tabia za tamaduni hii katika kununua huduma.
Kulea Kipaji cha Utengenezaji wa Michezo ya Video
Michezo yote mizuri inaanzia kwa watu na timu ambazo zimeitengeneza. Ni jambo moja kwa michezo ambayo haijatengenezwa Afrika kuchezwa, kama tunavyoona michezo inayomilikiwa na Wachina na Wamalta ya kubashiri lakini ni jambo linguine kukuza mfumo wa ikolojia ambao utamuwezesha mtengenezaji wa michezo wa ndani mwenye kipaji kukua zaidi Afrika. Tutazame hilo kama tunavyotazama ule msemo wa “Mpe mtu samaki/mchezo dhidi ya Kumfundisha mtu namna ya kuvua samaki/kutengeneza michezo”.
Nairobi Games Center
Hii ndiyo sababu Shapiro alitengeneza Nairobi Games Center. Kama mtandao wa WeWork ulivyo ila kwa ajili ya watengenezajiwa michezo wa Nairobi. Sehemu ya kufanya kazi kwa kushirikiana ambayo inawapa wanachama wake teknolojia za kisasa kama vile console za kisasa, maabara ya VR, na hata studio ya kunakili mwendo (Motion Capture Studio) kwa ajili ya kutengeneza michezo ya ndoto zao.
Lengo kuu ni kuandaa mazingira yatakayofanya utengenezaji wa michezo uweze kukua ndani ya Kenya. Sio tu kwa kutengeneza biashara kubwa sana ya uchapishaji wa michezo hiyo na kuwa na njia za usambazaji duniani au kuwa na umiliki wa michezo iliyotengenezwa ndani ya kituo (Shapiro anatuhakikishia kwamba Usiku haichukui umiliki wowote katika miradi ya watengenezaji) bali ni kwa kuwapa vifaa vya kisasa vya utengenezaji wa michezo kwa watengenezaji wabunifu waliojificha maeneo mengi ya Afrika. Watu wenye ndoto za kutengeneza michezo na hawana vitendea kazi muhimu lakini wana akili na uwezo wa kufanya hivyo.
Kwa sehemu kubwa, kitu ambacho Shapiro anajaribu kukifanya ni sawa alichokifanya Singapore. Wakati ule hakuwa akipambana kuanzisha Kampuni ya Matangazo ya Kidigitali kubwa Mashariki mwa Asia kote. Alichotaka tu ni kuanzisha sekta ya Matangazo ya Kidigitali kwanza na kisha faida zingepatikana zenyewe kutokana na lengo hilo.
Kwa hiyo Shapiro na Usiku Games wanafaidika na nini? Zaidi ya kutimiza ndoto za Wakenya wengi ambao wanataka dunia yao iwe na michezo mingi. Kiuhalisia, Usiku inaanza kujikita kama walinzi wa bara la Afrika. Pale watu kama Microsoft au Sony watakapotaka kuwekeza katika soko linalokua kama soko la Kenya, watahitaji kwanza kupita kwa Jay na timu yake.
Na ndiyo maana kipindi Phil Spencer [Mkuu wa Michezo Microsoft] akitembelea Nairobi, na amewahi kutembelea mara kadhaa kabla ya COVID, yeye na Shapiro hufanya maongezi. Kwa ari ile ile kama ya Kituo cha Michezo Nairobi, Microsoft inawekeza zaidi katika mafunzo ya open source ambayo yanahusisha Microsoft Azure Cloud.
Kwenye Upeo wa Macho
Marekani
Kutengeneza mazingira yanayojitosheleza ya kampuni za Kiafrika zinazotengeneza na kuchapisha michezo ni chachu inayohitajika ili masoko yaweze kukua yenyewe. Lakini uwekezaji mdogo kutoka nje sio jambo baya. Itakuwaje na kutokea wapi?
COVID imeathiri uchumi wa makampuni ya michezo yaliyo kwenye soko la hisa kwa namna 2.
Kwa upande mmoja mzuri, idadi ya watu wanaocheza michezo haijawahi kuwa kubwa kama sasa kwa sababu ya karantini zilizopo duniani kote. Watu wengi zaidi wanacheza michezo zaidi kwa muda mrefu zaidi na kutumia hela nyingi zaidi kwenye michezo hiyo.
Ubaya ni mfano unaowekwa. Inakuwaje makampuni kama Electronic Arts au Activision Blizzard yakaendelea kusukuma gurudumu mbele wakati dunia nzima taratibu inajaribu kurudi hali yake ya “kawaida”? Watawezaje kuendelea kuwapa wawekezaji wao ukuaji huu mkubwa kama walivyozoea kwa mwaka huu? Shapiro anaamini kwamba Afrika ndilo jibu la swali hilo. Kama mahitaji katika masoko ya magharibi, Ulaya au Asia yakishuka baada ya COVID kupita, wachapishaji wakubwa wanaweza kuhitaji kujitangaza kwenye masoko ya Afrika, kutengeneza michezo inayofunguka katika vifaa vyenye uwezo mdogo au kununua Studio ya Kiafrika ili kuhakikisha wanatengeneza michezo iliyo karibu zaidi na tamaduni hizi.
China
Kama ilivyotajwa hapo juu, miundombinu ya 4G inayozidi kuenea Afrika ni ya kisasa na gharama nafuu, je Afrika ina mpango gani na 5G? Makampuni ya teknolojia ya Kichina. Haswa marafiki zetu katika makampuni ya simu ya Kichina na yanayotengeneza vifaa vya ndani vya watumiaji, Huawei, ambao wanaiona Afrika kama sehemu ya utafiti, na fursa ya kusambaza mitandao ya simu katika bara kwa gharama ndogo, na kasi kubwa. Sio njia rahisi kwa sababu ya hofu juu ya faragha na kutumia vibaya programu za kutambua watu kwa sura(facial identification software) au kufuatilia mienendo ya watu (geo-location tracking) hutibua viongozi wa serikali nyingi za Afrika.
Zaidi ya uwekezaji wa majengo, Shapiro anatarajia wasaidizi wengi zaidi chini kutoka katika makampuni kama vile Tencent. Ofisi za mikoa na kuajiri kwa wingi kunaweza kutokea kwa miji mingi ya Afrika iliyoendelea. Kama zilivyo tamaduni za Kituo cha Michezo Nairobi, binafsi kimsingi naona ni jambo zuri. Kutoa kazi za kiteknolojia za ubora wa juu, zinazolipa vizuri sana kwa Waafrika itakuwa ni jambo litakalojenga zaidi mahusiano mazuri kati ya Afrika na China katika ulimwengu wa mbeleni. Sitashangaa kama wakazi wengi wa Afrika walioondoka na kwenda China kwa ajili ya masomo ya vyuo vikuu wakirudi baada ya kuhitimu na kuishia kufanya kazi katika makampuni kama vile Tencent, Baidu au Alibaba.
China yazidi serikali za magharibi kwa Ufadhili wa masomo Afrika
Operating Systems
Athari chanya za simu aina ya “feature phone” zimeonekana kwa muda sasa. Kwa ambao hawafahamu: ‘Feature phone’ ni aina ya simu ya mkononi ambayo ina kazi nyingi zaidi ya simu ya mkononi ya kawaida lakini haiko sawa na simu janja. Feature phone zinaweza kupiga na kupokea simu, kutuma ujumbe mfupi wa maandishi na kutoa kufanya baadhi ya kazi zinazoweza kufanywa na simu janja kama vile kutembelea intaneti. Zimekuwa msaada mkubwa sana katika nchi zinazoendelea, zikiwapa wananchi wake njia salama, ya gharama nafuu ya kutembelea intaneti kwa haraka.
Shapiro alinionyesha ‘extension’ katika wazo la ‘feature phone’ ambalo lilinishangaza sana – kitu kinachoitwa KaiOS. Tazama video iliyopo chini kupata muhtasari wake:
KaiOS imesafisha APAC miaka hii ya karibuni (ipo katika vifaa zaidi ya 150 milioni India pekee) huku sehemu kubwa ya shughuli zao zikitokea Hong Kong. Hivi ni vifaa kamili, sio feature phones, kwa bei ndogo (~$20 USD kwa kila kifaa). OS inatumika katika vifaa 51. KaiOS inakuwezesha kuingia katika Kai Store, soko la app za simu kama ilivyo Google Play au App store lenye app nyingi maridadi kama vile Facebook, Youtube na WhatsApp.
Tofauti ndogo ni kwamba KaiOS inatokana na HTML 5, inayowezesha kiasi kidogo cha uchezaji wa michezo lakini bado ni cha kushangaza. Ni kwa sababu hii iliyofanya Usiku games kutengeneza michezo yake kwa kutumia HTML 5 kwa jitihada za kuwafikia wachezaji kwenye vifaa vyao walivyonavyo (au watakavyovimiliki hivi karibuni).
Kupata kozi fupi ya utambulisho juu ya HTML 5 – tazama chini!
Kufunga
Chapisho hili ni moja kati ya chapisho langu pedwa zaidi nililowahi kuandika.
Kujifunza namna Afrika, mahali ambapo hata mimi najutia kupabagua kiuchumi wakati mwingine, panavyokua katika namna nyingi na nzuri kwenye eneo la michezo ni jambo linalotia matumaini. Ndiyo nimevutiwa na hatua zilizopigwa na watu, mienendo ya michezo, vifaa, program, uwekezaji wan je, elimu na mambo mengi. Lakini kuna jambo lingine. Jambo ambalo linanivutia zaidi – cheesiness inakuja!
Kumbuka kwamba mapenzi ya watu juu ya michezo haitegemeani na tamaduni lakini kwa wakati huo huo imejaa utamaduni na ni ushahidi tosha juu ya namna michezo inavyoweza kuunganisha watu. Ukweli wa kwamba uti wa mgongo wa michezo ya video iliyotokea kupendwa kama vile 2048 unaweza kufanya kazi hata Afrika ni vizuri sana. Mpaka ukahitaji kubadilishwa ili uweze kuendana na eneo fulani la wachezaji ni vizuri zaidi. Inaonyesha jinsi kila mtu yuko sawa katika kupenda michezo ya video, lakini wakitofautiana kwa namna wanavyoipokea – na hiyo ni kwa mtazamo wa mchezaji wa michezo ya video tu.
Katika upande wa utengenezaji, kama mtoto wa miaka 16 kutoka Senegal aliye na Unity Game Engine, kama ilivyokuwa kwangu nilipokuwa katika chumba changu cha kupanga kule Vancouver, anatumia nyenzo sawa, na kukutana na kasoro sawa na ana ndoto sawa, lakini tofauti za mchezo anaotaka kutengeneza ni wazo linalovutia.
Kama unataka kumfuatilia Jay Shapiro anachokifanya, mtazame katika Racket ambapo anaongelea mambo yote yanayohusiana na sekta hii ya michezo ya video ya Kiafrika!
Kama unataka kufuata Usiku Games, tembelea kurasa zao za kijamii zilizo hapo chini!